MWANGA Kikao
cha kujadili maendeleo ya kata ya Lembeni (WODC), wilayani Mwanga mkoani
kilimanjaro, kimemwagiza Mtendaji wa kijiji cha kisangara Josephat Rajabu Kayanda ifikapo tarehe 15 julai 2014
bomba la maji la kitongoji cha Lengurumo liwe limeunganishwa na shimo la choo
katika shule ya msingi kisangara liwe limekamilika.
Agizo hilo la kikao cha WODC cha julai 03, mwaka huu
limekuja baada ya kubainika kutotekelezwa kwa maazimio ya kikao kilichopita
kilichotaka kujua watu waliokata bomba linalopeleka maji kitongoji cha
Lengurumo wamepatikana na bomba hilo kuwa limeshafanyiwa matengenezo,ambapo
Mtendaji huyo alikiri kutofanikiwa kuwakamata wahusika na bomba kutofanyiwa matengenezo kutokana na
ukosefu wa fedha.
Kayanda amefafanua kwamba imekuwa vigumu kuwakamata
waharibifu hao wa miundo mbinu kwa kuwa hufanya uharibifu huo usiku, na kuhusu
matengenezo ya bomba amedai hawana pesa ambapo pia hata wilayani alipofuatilia
tatizo lilikuwa ni ukosefu wa pesa,naye Bwana maji wa kata ya Lembeni Awadhi
Mussa,alipoulizwa alionekana kutoa majibu asiyokuwa na uhakika nayo hali
iliyoonyesha kuna uzembe ndani yake.
Wajumbe katika baraza hilo kwa nyakati tofauti,wameonekana
kutoridhishwa na majibu ya Bwana maji wa kata aliyeonekana kutokujua hata
gharama za matengenezo ya bomba lililovunjika pamoja na sababu za ukosefu wa
fedha kwa kile walichohoji kuwa kazi ya bodi ya maji ni nini?ambapo waliwataka
siku ya zamu ya maji kuelekea lengurumo ambayo ni kila jumatatu,mabomba yote ya
kisangara na mangara yafungwe ili maji yafike.
Aidha kikao hicho cha WODC, kimetaka ratiba ya maji ya
kijiji hicho ifuatwe kama inavyostahili na funguo za maji za taasisi ziwekwe
ofisi ya kijiiji na kutoa wito katika uongozi wa vijiji vyote vya kata ya
lembeni kuwa makini na bodi zao za maji na kuzitaka bodi hizo kuacha ukiritimba
katika kuwahudumia wananchi.
Wakazi wa ustawi wa jamii katika kitongoji cha lengurumo
hulazimika kutembea umbali wa takribani kilometa saba kufuata maji katika
kijiji cha kisangara kwa matumizi ya nyumbani, kwa kutumia usafiri tofauti
tofauti ikiwemo punda,bodaboda na magari ;Huku Chuo cha Ustawi wa jamii cha
kisangara kikitumia kiasi cha shilingi milioni moja kwa wiki mbili sawa na
sh,12milioni kwa miezi sita kununua maji kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho.
Mwenyekiti wa kijiji cha kisangara Selemani Said akisoma
tarifa ya kijiji katika kikao hicho amesema Waziri wa maji na Mbunge wa wilaya
ya mwanga Prof. Jumanne Maghembe aliagiza hadi julai,15 mwaka huu mradi wa
visima virefu utakuwa umekamilika na wananchi watapata maji.
No comments:
Post a Comment