Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 16, 2014

TASAF YATENGA MILIONI MIA NNE KUSAIDIA FAMILIA MASIKINI WILAYANI ROMBO

ROMBO mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF umetenga jumla ya bilioni mia nne (400,000,000) kwaajili ya mpango wa kutokomeza umaskini kwa watanzania ikiwa ni awamu ya tatu ya mradi huo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa kujenga uwezo kutoka TASAF Faraji Michael, wakati wa warsha ya siku tano, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro yenye lengo la kujenga uelewa kwa wadau juu utekelezaji wa mpango huo.

Alisema kuwa fedha hizo zimetegwa kwaajili ya kuwafikia watanzania wenye hali ya umaskini uliokithiri na kwamba halmashauri 161 zitafikiwa na mpango huo .

Aidha alisema kuwa mradi huo utawanufaisha watanzania na kufikia kaya zote ambapo utawasaidia watanzania kuongeza kipato na kupunguza umaskini, kutoa ajira, kujenga na kuboresha mundombinu  inayolenga sekta ya afya, maji na elimu.

Michael alisema mbali na kufikia kaya zote maskini pia mpango huo umelenga kumfikia mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma zote ikiwemo elimu na matibabu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Rombo Elinasi Pallangyo, alisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya ya Rombo ni maskini  kutokana na wengi wao hukosa hata mlo mmoja wa siku.

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakitegemea kilimo na kwamba maeneo wanayolima ni madogo na hayakidhi mahitaji hivyo migogoro ya ardhi ni mingi jambo ambalo limekuwa likiendeleza umaskini miongoni mwa wananchi wa Rombo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya hiyo aliwataka watendaji watakao husika katika uteuzi wa kaya maskini  kufanya kazi kwa uaminifu ili lengo la mradi huo liweze kufanikiwa na kuwasaidia watanzania kuinua uchumi wao.

No comments:

Post a Comment