Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 9, 2014

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUBORESHA VYUO VYA WAUGUZI HAPA NCHINI

MOSHI serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaendelea kuviboresha vyuo vyote  vinavyofundisha wauguzi hapa nchi ili kuwa na uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi kuliko ilivyo sasa.

Hayo yamesemwa na waziri wa Afya, Dkt Seif Mohamed Rashid, wakati
alipokuwa akikabidhi vitanda 18, magodoro pamoja na Mashuka 90 kwa halmashauri  ya Same, ajili ya wodi za wamama wajawazito, wa kata 16 za jimbo la same
Mashariki, halfa ambayo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Waziri huyo,  amesema mkakati uliopo kwa sasa katika wizara yake ni
kuviboresha vyuo hivyo ili kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi kuliko ilivyoa sasa ambapo vyuo hivyo vinachukuwa wanafunzi 40 hadi 50, kwa mwaka  na kwamba kuboreshwa kwa vituo hivyo vitaweza kuchukua wanafunzi 400 kwa mwaka.

Amema huduma za afya kwa ujumla wake bado zina gharama kubwa,
na kwamba kwa nchi ya Tanzania wastani wa mtu mmoja anatumia kiwango cha dola 41, za kimarekani kwa mwaka kujitibu, ambapo kwa  marekani wanatumia wastani wa kila mtu mmoja  dola 6,000 hadi  9000, kwa mwaka, na kuwaomba wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambao utaweza kupunguza matatizo yanayowakabili.

Awali Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Vick Bishubo, amesema wametoa
msaada wa Vitanda, Mashuka na Magodoro, vikiwa na jumla ya shilingi milioni 15,  ili kuweza kuokoa maisha ya wa Mama ambao walikuwa wakijifungulia chini.

Amesema sekta ya afya imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa vitanda vya kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati, hivyo Benki ya NMB, imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.3 kwa mwaka 2014 ili kusaidia jamii katika Nyanja ya Elimu, afya na Michezo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Same Mashariki, Anna kilango, licha
ya kuipongeza Benki ya MNB, kwa kutoa msaada huo, ambao utapungua adha ya wajawazito kujifungulia majumbani, pia ameiomba serikali kuwapatia watumishi wa afya ili waweze kutoa huduma iliyo bora.

No comments:

Post a Comment