WANANCHI wa kata ya tungi manispaa ya morogoro
wameulalamikia uongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MORUWASA
kwa kutowapatia huduma nzuri ya upatikanaji wa maji safi katika maeneo yao.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema pamoja na na
kuwepo na mabomba lakini ni kipindi kirefu sasa wamekuwa wakitumia maji ya
vidimbwi yaliyotuama vilivyoachwa na maji ya mvua za masika ambavyo si salama
kwa matumizi ya binadamu kutokana na mabomba hayo kutotoa maji.
Voxpops…wananchi
Aidha wamelalamikia pia bei ya Ankara za maji kwani zipo juu
tofauti na huduma ya maji wanayoipata nah ii wamesema inatokana na wasoma mita
kutoa taarifa za uongo kwa kuandika kiwango kikubwa cha pesa hivyo kuwasababishia
baadhi ya watu kuondoa mita majumbani mwao.
Kwa upande wake diwani wa kata ya tungi Deogratius Mzeru
amesema kufuati hali hiyo amefika mara nyingi kuonana na uongozi wa muruwasa
ili kuzungumzia hatma ya suala la maji katika kata yake ambapo amejibiwa ni
jukumu la wananchi kuchangia fedha ili kuunganishiwa bamboo kubwa la maji.
Insert..deogratius Mzeru-diwani kata ya tungi.
Tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika manispaa
ya morogoro limekuwa kuwa sugu,pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na
mbunge wa jimbo hilo mheshimiwa abdul azizi abood kulifuatilia kwa ukaribu na
hata kulifikisha bungeni.
No comments:
Post a Comment