MOSHI wakazi wa
kijiji cha Kitandu kata ya Uru kusini wilayani ya Moshi mkoani kilimanjaro
wamemtaka mwekezaji wa shamba kubwa la kahawa lenye hekari 555 la kifumbu/kate
kutekeleza makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa uwekezaji.
Wananchi hao walitoa agizo hilo katika
mkutano mkuu wa serikali ya kijiji uliofanyika tarehe 5 Augasti 2014 na
kuudhuriwa na wawakilishi
wa mwekezaji wa kampuni ya Kilimanjaro Plantation LTD. (KPL).
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Dominick Mushi, alisema kampuni hiyo imeshindwa
kutekeleza mkabata huo kwa kushindwa kuwapatia huduma za kijamii wananchi kwa
miaka 20.
Mushi alisema baadhi ya huduma hizo ni
pamoja na maji, elimu, afya, barabara, ajira kwa wananchi na kudorora kwa
ushirikiano kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wananchi wa kijiji hicho.
Aidha alisema, kwa muda mrefu serikali
ya kijiji ilikuwa inauomba uongozi wa kampuni hiyo kukutana na wananchi
kujadili mustakabali wa mkataba huo lakini viongozi wa kampuni wamekuwa hawatoi
ushirikiano.
Alisema kwa zaidi ya miaka 20 ni mara ya
kwanza kwa viongozi wa kamapuni hiyo kukaa na wananchi na kusikiliza kero zao
zinazo wakabili likiwemo suala zima la maendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni
hiyo Jacob De Haan aliahidi kuwasilisha hoja za wananchi hao kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Volker Schuckert ambaye kwa sasa yuko nchini
Ujerumani kwa mapumziko na kwamba matumaini yake kuwa zitafanyiwa kazi
kwa mujibu wa mkataba.
Mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa
kampuni hiyo Shaaban Deogratius alikiri uhusiano mbaya uliopo kati ya pande
hizo na kuaahidi kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na kuondoa tofauti
zilizojitokeza.
Shaaban alisema, katika hatua za awali
aliahidi ajira 25 za ulinzi kwa vijana watakaomaliza mafunzo ya mgambo katika
kijiji hicho ili kuziba pengo la walinzi waliopo ambao baadhi yao ni wazee na
wengine hawana sifa.
No comments:
Post a Comment