MOSHI aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), mkoani Kilimanjaro, Thomas
Ngawaiya, ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha ubunge cha Moshi
Vijijini, mkoani Kilimanjaro, katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Ngawaiya
ambae aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kati ya mwaka 2000 na 2005,
ametangaza nia yake hiyo, akiwa nyumbani kwake Kibosho, ambapo
amesema lengo kuu la nia yake hiyo ni kuharakisha maendeleo katika
jimbo hilo.
Amesema mwaka 2005 hakufanya hivyo kwa vile wakati
akipewa ushauri huo tayari alishaamua kugombea ubunge wa jimbo la
Moshi Mjini na kushika nafasi ya tatu katika kura za maoni ndani ya
CCM.
Ngawaiya amesema kuwa kingine kilichompa msukumo wa
kufanya hivyo ni kuwa jimbo la Moshi Vijijini limekosa mtetezi wa
ngazi hiyo haswa katika sekta ya kilimo cha kahawa na kwamba
ameazimia kuhakikisha zao hilo linarudia hadhi yake ya awali kwa
manufaa ya wakulima wake.
Aidha amesema aliasisi mradi wa
ujenzi wa barabara za maeneo ya jimbo hilo kwa kiwango cha lami na
kwamba wananchi wa eneo hilo ambao ni wapiga kura ndiyo mashahidi
wake.
Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na Dk. Cyril Chami, wa
CCM; mbali na Ngawaiya, wengine ambao wameshaonyesha nia ya kuwania
kiti hicho ni pamoja na aliekuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno
Malisa, ambapo taarifa zingine zisizo rasmi zinaonyesha ya kuwa
mbunge wa viti maalum
kupitia Chadema,Lucy Owenya, pia anatarjia
kuwania kiti hicho.
No comments:
Post a Comment