Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 27, 2015

Mtoto wa miaka mitatu akutwa akiwa amefariki dunia baada ya kutumbukia chooni

KILIMANJARO Mtoto wa Miaka Mitatu anayefahamika kwa jina la Prenes Ardo ametumbukia chooni na kufariki dunia. Tukio hilo lla kusikitisha limetokea katika kijiji cha Sanya hoyee, Mabanzini Wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro.


Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Jemse, alisema kuwa alisikia watu wakipiga yowe na kuomba msaada ambapo alifika eneo hilo na kuambiwa kuwa kuna mtoto amepotea hivyo wananchi wote wakamtafute mtoto huyo.

Alisema baada ya kumtafuta mtoto huyo sehemu mbalimbali kwa muda mrefu, katika hali ya kusikitisha waliukuta mwili wa mtoto huyo ukielea katika maji machafu ya choo, ambacho ni choo kilichopo jirani na familia ya mtoto huyo, ambapo alikua tayari ameshafariki.

Mama wa mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Estar Ardo, alisema kuwa yeye alikuwa katika shughuli zake na aliporejea nyumbani mida ya saa tisa alasiri, hakumkuta mwanae ndipo alipoanza kumtafuta, lakini bila mafanikio ilipofika mida ya saa kumi na mbili alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Kijiji hicho Moses Munuo.

Ndipo mwenyekiti wa kijiji hicho alipopiga mbiu, ikiwa ni ishara ya jambo hatari limetokea katika kijiji hicho. Watu wakajitokeza na kukusanyika ili kufahamu kilichotokea. Mwenyekiti akawaeleza kuhusu kupotea kwa mtoto huyo na watu wote wakaanza zoezi la kutafuta, mida ya saa moja jioni mtoto huyo akakutwa katika choo cha jirani akiwa amesha fariki.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho Moses Munuo alisema ni kweli na kwamba mwili wa mtoto huyo upo katika chumba cha kuifadhia maiti katika Hospitali ya Kibongoto. Alisema tukio hilo lilizoa simazi na masikitiko makubwa kwa wananchi waliofika katika eneo hilo, pia amewataka wananchi kutokuacha mashimo wazi kwani ni hatari sana.

Na Joshua Fanuel 

No comments:

Post a Comment