Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 27, 2015

Safari ya matumaini ya Mheshimiwa Edward Lowassa yapata wadhamini 33,780 mkoani Kilimanjaro


Meshimiwa Edward Lowassa akiwahutubia baadhi ya wananchi mkoani Kilimanjaro waliomdhamini na kupata nafasi ya kuingia ndani na jengo la CCM mkoa

 Mheshimiwa Lowassa akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mkoani Kilimanjaro na viunga vya jirani waliojitokeza kwa wingi nje ya jengo la CCM mkoa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, June 18, 2015.

Maelfu ya wananchi waliohudhuria katika safari ya matumaini ya Lowassa nje ya jengo la CCM mkoa.


Na Joshua Fanuel.
KILIMANJARO Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mheshimiwa Edward Ngoyani Lowassa aliyeianza safari ya matumaini katika uwanja wa michezo wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha Mei 30, 2015, kwa kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumteua kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama tawala cha CCM.

Siku ya jana June 18, 2015 aliendelea na ziara ya yake ya kusaka wadhamini mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo kwa taratibu za katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mgombea anatakiwa kupata jumla ya wadhamini 450, katika mikoa 15 ya Tanzania ili kukidhi vigezo vya kupewa ridhaa ya kugombea urais.

Edward Lowassa ambaye anaonekana kuvunja rekodi ya kupata wadhamini wengi kwenye kila mkoa anaopita kusaka wadhamini jana ameendelea kulidhibitisha hilo kwa wadhamini aliowapata katika majimbo saba ya mkoani Kilimanjaro, ambapo hali ilikua hivi, Jimbo la Moshi Vijijini 11564, Jimbo la Rombo 6615, Jimbo la Hai 1854, Jimbo la Siha 9860, Jimbo la Moshi Mjini 1184, Jimbo la Same 1600, Jimbo la Mwanga 1103. Jumla ya wadhamini katika majimbo yote ni 33,780.

Lowassa aliwashuuru sana wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro waliomdhamini na wale walioacha shuhuli zao na kwenda kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini, kati ya mambo ambayo aliendelea kusisitiza katika hotuba yake ni kwamba anauchukia sana umasikini na akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi ya Tanzania atahakikisha anatokomeza umasikini.

Aliwaahidi wakazi wa mkoani Kilimanjaro kuwa endapo atapewa ridhaa na kuiongoza nchi hii atajitahidi mwezi wa kwaza wa utawala wake aanze na mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha amefufua viwanda vilivyofungwa kwa hila, ili vijana waweze kupata ajira na kuondokana na umasikini uliokidhiri.

Aliendelea kuwasisitizia kwa wale wenye sifa za kujiandikisha waende kujiandikisha mapema kwenye vituo vilivyo karibu yao ili siku ya uchaguzi ikifika waweze kumchagua kiongozi wanaompenda na maana kiongozi anachaguliwa na wananchi wenyewe na kuendelea kumshangilia bila kwenda kujiandikisha ni kazi bure.

Pia Mhesimiwa Lowassa alisema endapo atachaguliwa kuiongoza nchi ya Tanzania atahakikisha wananchi wote kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida wanakimbia mchakamchaka katika kuufukuza umasikini na kuukaribisha utajiri, na alisisitiza kuwa kwa yeyote ambaye hatakua tayari kukimbia mchakamchaka katika kuleta mafanikio atamuweka pembeni na kupisha wale walio tayari kwa mchakamchaka kuendelea kuijenga nchi ya Tanzania ambayo itakua nchi ya asali na maziwa.

No comments:

Post a Comment