Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 19, 2015

Taasisi ya African Muslim Agens Mkoani Kilimanjaro inatarajia kufuturisha makundi mbalimbali ya Kiislam

KILIMANJARO taasisi ya African Muslim Agens yenye makao yake Kaloleni, Mkoani Kilimanjaro inatarajia kutumia zaidi ya Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya kufuturisha makundi mbalimbali ya Kiislamu Mkoani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Msikiti wa Riadha uliopo Manispaa ya Moshi Mkurungenzi wa Taasisi hiyo Aly Adamu, alisema fedha hizo zitatumika kusambaza futari katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu.

Adamu alisema kuwa wazo la kufuturisha lilikuja baada ya kuona baadhi ya Waislamu wakihangaika kutafuta futari wakati wa kufuturu na wengine hawana uwezo wa kununua futari.

Alisema kuwa Taasisi yake imekuwa ikitekeleza mpango huo miaka mingi na kila mwaka wanakuwa wakiongeza maeneo mengine mapya ya kufuturisha.

Aidha alibainisha kuwa makundi yatakayo nufaika ni pamoja na Misikiti 10, vyuo 4, vituo vya kulelea watoto yatima 2, pia hata wafungwa waio katika gereza ya Lukaranga Moshi.

Sambamba na hilo aliwataka Waislam kusoma Kuruan kwa wingi katika mwezi wa Mfungo wa Ramadhani, kwani mwezi huu ni mwezi wa kuchuma na kuwataka kuacha kupoteza muda.

No comments:

Post a Comment