JESHI la polisi mkoani kalimanjaro linamshikilia
Masha Huruma (28)
mkazi wa pasua kwa kosa la kumgonga
omari Chikira(60) wakati akivuka barabara kuelekea upande wa pili, na
kufariki dunia.
Kamanda wa polisi Robert Boaz, alisema tukio hilo
lilitokea juni 23
mwaka huu majira ya saa10:30 jioni katika barabara ya market street
manispaa ya moshi, ambapo mtuhumiwa alikuwa
akiendesha gari lenye
namba za usajili T 749 AVT Toyota corolla.
Alisema mzee huyo ambaye aliwahi kuwa katibu tawala
wa mkoa wa
Kilimanjaro alijeruhiwa sehamu mbalimbali za mwili
ambapo alisema ni
kichwani,kifuani na kuvunjika miguu, ambapo
alifariki dunia wakati
akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC
.
Kamanda boaz alisema, mtuhumiwa huyo baada ya
kutenda kosa hilo
alikimbilia kusikojulikana lakini baada ya uchunguzi alikamatwa na
kufikisha katika kituo cha polisi cha mjini moshi.
Alisema mtuhumiwa huyo atafikisha mahakamani pindi uchunguzi utakapo kamilika ili kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Kamanda amewataka watumia vyomo vya moto vya
barabarani kufuata sheria na kuwa waangalifu wakati wakiwa barabarani.
No comments:
Post a Comment