Polisi wamesema zaidi ya watu wanane wamejeruhiwa kufuatia shambulio hilo lililotokea saa nne, Jumapili usiku.
Shambulio hilo limejiri siku moja baada ya ubalozi wa Marekani nchini
Kenya kuonya kuwa ''kulikuwa na tisho la kutokea shambulio la kigaidi''
katika eneo hilo.
Mapema wiki hii, maafisa wa polisi wa Kenya waliwakamata raia wawili wa
Iran waliotuhumiwa kuhusika na mtandao wa kigaidi unaopanga kutekeleza
mashambulizi mjini Mombasa.
Siku ya Jumamosi, polisi katika mji mkuu Nairobi, walisema kuwa walipata vifaa vinavyo shukiwa kutumika katika kutengeneza bomu.
Mkuu wa polisi wa mkoa wa pwani, Aggrey Adoli, hata hivyo amesema hawezi
kuhusisha moja kwa moja shambulio hilo la Mombasa na ilani iliyotolewa
na Marekani.
''Taarifa tulizopata ni kwamba kifaa hicho ambacho tunashuku ni gruneti,
kilirushwa na mtu mmoja aliyekuwa akiburudika kwenye baa hiyo.
Hatukuweza kumnasa mtu huyo lakini tunaendelea na uchunguzi,'' Adoli
aliambia kipindi cha Amka na BBC.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo amesema kuwa , wakati mlipuko huo
ulipotokea, baa hiyo ilikuwa na wateja wengi waliokuwa wakitizama mechi
ya robo fainali kati ya Uingereza na Italia, katika michuano ya kombe la
taifa bingwa bara Ulaya.bali na Marekani, ubalozi wa Ufaransa mjini Nairobi pia umeonya raia wake '' kuwa waangalifu'' wakiwa katika mji huo wa Mombasa.
Marekani iliwatahadharisha raia wake kutozuru Mombasa hadi Julai mosi.
Mwezi Mei, mtu mmoja aliuwawa wakati kilipuzi kiliporushwa ndani ya mkahawa mmoja mjini humo.
Kumekuwa na msururu wa mashambulizi ya gurunedi tangu Kenya ilipopelekwa
wanajeshi wake nchini Somalia kuwasaka wapiganaji wa kundi la kigaidi
la Al- Shabab, mwezi Oktoba mwaka jana.
Chanzo:bbc
No comments:
Post a Comment