Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 28, 2012

VILIO VYATANDA KWA WAHITIMU WA UHIFADHI WA WANYAMAPORI CHUO CHA PASIANSI, MWANZA...!


Wanafunzi wa chuo cha Pasiansi, Mwanza wakiwa katikati ya pori 
la serengeti, katika zoezi la kufunga na kufungua silaha.


 

Hawa ndio wahitimu wa chuo cha Pasiansi, Mwanza, wa June 2012.

Chuo cha taaluma ya wanyamapori pasiansi, kinachopatikana mkoani mwanza, 
wilaya ya ilemela. Chuo hiki chenye sifa ya kutoa askari wahifadhi waliopewa 
mafunzo ya silaha, kwata chini ya kamishina mstaafu wa jeshi la polisi 
Venance Tossi ambaye pia anaendesha mafunzo ya askari waajiriwa ndani ya 
idara ya wanyamapori, na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro , na tabia mbalimbali 
za wanyama. Pia chuo hiki ambacho kimetoa idadi kubwa ya askari ambao 
wameajiriwa katika idara ya wanyamapori, mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro na 
hifadhi za taifa miaka miwili iliyopita na kurudi nyuma. Lakini pamoja na kutoa 
askari wenye ujuzi wenye mbinu za kijeshi bado ajira kwa askari hawa limekuwa 
tatizo kubwa kiasi kwamba inahatarisha kwa askari hawa kujiingiza kwenye ujangiri, 
ujambazi na mambo mengine yasiyofaa katika jamii kwa ujumla.
Mwaka 2010 kozi na. 45 na. 3 ya mafunzo ya astashahada ya awali ngazi ya cheti yaani 
Basic Technician Certificate in Wildlife Management na mafunzo ya stashahada 
ngazi ya cheti yaani Technician Certificate in Wildlfe Management ndiyo kozi za 
mwisho kuajiriwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.
 Kozi ziliyofuata na. 46 na 2 ya astashahada ya awali na stashahada ngazi ya cheti yaani 
Basic na Technician Certificate in Wildlife Management ambazo zina idadi kubwa ya
 askari ambao hawajaajiriwa mwaka wa pili umeanza sasa bado wapo nyumbani. Kutokana 
na chuo kupata sifa nyingi idadi ya wanafunzi askari watarajiwa imezidi kuongezeka 
miaka inavyozidi kwenda hadi sasa kuna kozi na. 47 na 3 zote zipo nyumbani zinasubiria 
ajira. Mwezi wa 4 mwaka 2012 idara ya wanyamapori kupitia idara ya utumishi ilitangaza 
nafasi 130 za askari wahifadhi wanyamapori ngazi ya certificate cha kushangaza idadi 
kubwa ya watu walioitwa kwa ajili ya interview ni wale waliopitia vyuo vya mtaani 
visivyotambulika na serikali na kuacha askari wengi kutoka pasiansi. Wanafunzi hao 
walioitwa kwa ajili ya interview ni wale waliopitia vyuo vya tour guide.
Chuo cha taaluma ya wanyamapori pasiansi kipo chini ya idara ya wanyamapori na wao 
ndiyo wahusika waliotoa nafasi cha kushangaza wanachukuliwa watu ambao hata silaha,
kwata na ukakamavu hawana. Basi idara ingekifuta chuo kisitambulike ukizingatia chuo 
kinachaji ada kubwa ambapo wazazi wanajinyima ili kumlipia mtoto wakitegemea 
hakihitimu hataajiriwa. Ada ni 2,800,000/= kwa Basic Technician Certificate in 
Wildlife Management na 3,000,000/= kwa Technician Certificate in Wildlife Management.

Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya wanafunzi walio hitimu chuoni hapo ambao 
hawakupenda kutaja majina yao.. 

No comments:

Post a Comment