|
Saturday, 23 June 2012 11:03 |
MCHEZA filamu mwenye mvuto katika tasnia hiyo Jaqueline Wolper,amesema kuwa wanawake wanaweza bila kuwezeshwa,tatizo ni hawajiamini na hawapendani. Alisema si jambo la ajabu kuona mwanamke mwenzio anakuundia timu ya kukusema vibaya kwa chuki zake binafsi. Wolper alifunguka kuwa bado tunaamini kuwa wanaume ndio wanapaswa kuwa na mafanikio na ukiwa nayo, mwanamke mwenzao huanza kukuzushia kila aina ya jambo ilimradi tu kukuvunja moyo. "Wanawake kama tungekuwa tunapendana na kuamini mafanikio yetu sio lazijka yawe na mkono wa mwanaume nakwambia tungekuwa mbali lakini hatujiamini hata kwa vitu vidogo ambavyo wenyewe tunamudu kufanya"alisema Wolper. Wolper aliendelea kuonyesha masikitiko yake kwa kusema kuwa,wanaume wanaamini hakunba mafanikio bila kuwa na mwanamke lakini sisi hatujiamini wenyewe kwa nini wakati kwa kawaida mwanamke alizaliwa kiongozi. "Tangu enzi za Adam na Hawa mwanamke alikuwa ni kiongozi sio kwa maana ya mtawala lakini kwa maana ya kuwa na majukumu mengi ikiwemo nguvu ya kufanya kile anachokitaka na kufanikiwa kama hiyo haitoshi kwa hali ya kawaida mwanamke ndio mlezi wa nyumba na kujua kila kitu bila kujali anafanya kazi au laa"alisema msanii huyo mwenye sura ya kuvutia. Alimalizia kwa kusema kuwa kama wanawake wote wangeamua kupendana na kujiamini ha`ta kizazi chetu kilichopo na kijacho kingekuwa na maendeleo hivyo tuanze sasa kwani hatujachelewa. |
No comments:
Post a Comment