Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, June 24, 2012

JB afurahia tunzo za Bantu


Saturday, 23 June 2012 11:02

        Jakob Steven 'JB'
 
 

Kalunde Jamal
MCHEZA filamu, Jakob Steven 'JB',amesema kuwa kuwepo kwa tuzo za filamu ni nafasi pekee kwa wasanii kuonyesha umahiri wao kwa kufanya kazi zenye ubora unaotakiwa.

JB,alisema hayo alipokuwa kwenye uzinduzi rasmi wa tuzo za filamu hapa nchini zijulikanazo kama Bantu Film Awards,ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

Alisema kumekuwa na tabia ya kuandaa filamu zenye mvuto kwa kuangalia lakini zenye tafsiri mbaya ya kiingereza (Subtitle)kiasi cha kumfanya mtazamaji mwenye akili timamu kujisikia vibaya kuitazama.

Aliongeza kuwa ukiachilia tabia hiyo alikini kumekuwapo na tabia ya kuvaa mavazi yasiyo na maadili mema kwa jamii,bila kuangalia unacheza filamu ya aina gani.

Alifafanuwa kuwa kama unacheza nafasi inayohusu mavazi hayo sawa kama vile unaigiza ukahaba lakini sio mama wa nyumbani unaigiza umevaa mavazi ya ajabu,suala hili pia litaangaliwa kwa ukaribu zaidi.


"Ili kukomesha yote haya ni kuwepo kwa tunzo hizi ,ambazo zitakuwa ni changamoto kwa wasanii huku zikiwatia hamasa ya kufanya vizuri zaidi"alisema JB na kuongeza kuwa.

"Tutahakikisha zinakuwa na changamoto kubwa na nitaongea na watakaokuwa majaji kuangalia kwa kila picha na ubora wake na ziwepo kategory za kutosha ili kuweza kukosoa kwa mapana na marefu na lisiwe zoezi la kulipua"alisema.

Aidha alifafanuwa kuwa ili kuwapa moyo wahusika wa kuandaa filamu kwa maana ya maproducer,waandishi wa muongozo(Script),wapiga picha ,wanao waremba washiriki na wengine wote wanaohusika kwa namna moja ama nyingine wahusishwe kwa karibu katika tuzo hizo.

Nae muandaaji wa tuzo hizo Stuwart Kambona,alisema kuwa kwa kuanzia mwaka huu zitahusishwa filamu zote zilizowahi kuchezwa hapa nchini lakini miaka ijayo zitakuwa ni filamu za mwaka husika.

Kila kitu kinakwenda sawa na jinsi ya kushirikisha kazi zao ni kupitia kwa waandaji na wadau wa filamu kote nchini ambao watapendekeza ni filamu ipi inaingia kwenye hilo shindano na hatimae kupatikana mshindi wa jumla katika kila kategori.

"Hili sula litakuwa likifanyika kila mwaka kwa kuangalia filamu za mwaka uliopita,lakini mwaka huu tutahusisha filamu zote bila kujali ni ya mwaka gani na tumefanya hivi kama changamoto kwa wasanii kila mmoja ambaye yupo kwenye tasnia hii aingie ili miaka inayofuata awe na tamaa ya kuingia tena na kwa hiyo atajipanga kwa kutengeneza filamu nzuri na zenye maana."alisema Kambona.

No comments:

Post a Comment