Baadhi ya miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Seagull.
Baadhi ya wasafiri waliookolewa katika ajali hiyo.
MIILI 25 ya watu walifariki katika ajali ya meli ya Seagull iliyozama
jana imeokolewa kutoka majini. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es
Salaam kuelekea visiwani Zanzibar ilizama eneo la Chumbe jirani na
Zanzizar. Watu 145 walionusurika katika ajali hiyo wameokolewa wakati
watu 120 wakiwa bado hawajapatikana mpaka mwisho wa zoezi la uokoaji
lililofungwa jana jioni baada ya giza kuingia. Seagull ilikuwa na abiria
250, watoto 31 na wafanyakazi 9 ikiwa ni jumla ya watu 290. Chanzo cha
ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni dhoruba kali iliyotokea baharini wakati
chombo hicho kikiwa safarini. Zoezi la uokoaji litaendelea leo.
No comments:
Post a Comment