KATIKATI NI MWENYEKITI WA CHADEMA
MBEYA MJINI JOHN MWAMBIGIJA.
KATIKA
hali ya kusikitisha, Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya
ya Mbeya kimesema kuwa kitaendelea kuwaandamanisha vijana ambao
watapambana na vyombo vya dola huku wao wakiwa wamejificha na kuyaratibu
maandamano hayo.
Kauli
hiyo ya kutisha kwa mustakabali wa wafuasi wa chama hicho hasa vijana,
ilitolewa jana na viongozi wa chama hicho wilaya ya Mbeya Mjini katika
kikao chao na waandishi wa habari baada ya kuulizwa kuwa kwanini
wanayaratibu maandamano ambayo wao wanajificha.
Mwenyekiti
wa chama hicho wilayani humo John Mwambigija ambaye swali lilimlenga
moja kwa moja yeye kufuatia kauli zake zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi,
alisema kuwa mtindo huo ataendelea kuutumia ili yanapozidi na viongozi
wa Serikali wanapohaha yeye anaamuru vikosi vyake vingine kwa ajili ya
kuyarudisha nyuma maandamano.
''Ni
kweli mimi na viongozi wenzangu hatuwezi kuonekana katika maandamano
hayo ili kama Serikali inazidiwa tunayarudisha nyuma lakini katika
maandamano hayo hatuwatumi waandamanaji kuchoma moto au kuharibu mali za
watu labda inajitokeza kutokana na wao wenyewe kujitambua'' alisema
Mwambigija.
Majibu
hayo yalidhihilisha kuwa maandamano yanayofanywa chini ya uratibu wa
chama hicho na uongozi wake endapo yataendelea kufumbiwa macho na
Serikali yanaweza kuleta madhara makubwa siku za usoni.
Uongozi wa Mtandao huu wa chanzo chetu cha habari unatoa tahadhali hasa kwa vijana ambao wanaandamanishwa kuwa makini na njia zinazotumika na wanasiasa kwani madhara wanayoyapata wao ni faida kwa viongozi hao wa vyama na familia zao ambazo hawazipeleki katika maandamano hayo kutokana na kujua athari zake.
No comments:
Post a Comment