CHAMA Cha
Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha kimeendelea na mikutano yake ya kampeni katika
uchaguzi mdogo wa kata ya Daraja mbili
wilayani Arusha na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutochagua vyama vinavyohamasisha
vurugu,maandamano na mauaji.
Akihutubia
mwishoni mwa wiki iliyopita katika kampeni za uchaguzi huo zilizofanyikan
katika uwnaja wa Lamlawa mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha,Onesmo Ole Nangole
aliwaambia wakazi wa kata hiyo kwamba sifa ya mji wa Arusha imetoweka kutokana
na vurugu,maandamano na mauaji kurindima mkoani hapa.
Aliwaambia
kwamba Arusha umekuwa ni mji wa maandamano,vurugu na mauaji kana kwamba hauna
wakazi wazalendo na kuwataka wakazi wa kata hiyo kuwa makini na vyama
vinavyochangia matukio hayo.
“Arusha
umekuwa ni mji wa maandamano na vurugu kila kukicha kana kwamba hauna wenyeji
sifa ya mji wa Arusha imetoweka sasa kuweni makini na baadhi ya vyama
vinavyohamasisha vurugu”alisema Ole Nangole
Hatahivyo,alisema
kwa mujibu wa safu mpya ya uongozi wa CCM wilaya na mkoa ambayo imechaguliwa
hivi karibuni wana uhakika CCM itashinda uchaguzi huo na nyingine mbalimbali
kwa kuwa hakuna mamluki ndani yake.
Alisema
kwamba katika uongozi uliopita wa CCM mkoani hapa kulikuwa na mamluki ndani ya
chama chao ambapo waligundua mchana watu hao walikuwa CCM na usiku wapinzani
hivyo wamewatimua wote ili kukisafisha chama chao.
“Tulikuwa na
wana CCM mchana usiku wapinzani lakini tumewatimua wote huu uongozi wa sasa
umejipanga kuhakikisha tunashinda chaguzi mbalimbali mkoani Arusha nina na
imani na tembeeni vifua mbele wana CCM”alisisitiza Ole Nangole
Naye,mgombea
wa udiwani kupitia chama hicho,Phillip Mushi akinadi sera zake aliwaambia wakazi
wa kata hiyo wamchague kwa kuwa anatambua kero na mahitaji yao kwa kuwa yeye ni
mkazi wa kata hiyo.
Aliwaambia
ya kwamba endapo wakimchagua atashirikiana nao bega kwa bega kutafuta maeneo ya
kufanyia biashara hususani kwa
wafanyabishara ndogondogo maarufu kama wamachinga.
Mushi,alisema
kwamba pindi wakimchagua atajitahidi
kukarabati shule za sekondari na msingi
za daraja mbili ili kuzifanya kuwa za
kisasa huku akihaidi kumalizia ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ambayo imekwama hadi sasa.
Naye,diwani
wa kata ya Terat,Julius Ole Sekeyan alitumia muda wake jukwaani kumshambulia
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwamba ndiye aliyehusika kuwahamasisha
wamachinga kuvamia eneo la kiwanja cha Ermoil hivi karibuni na kulaani tukio hilo kwamba ipo siku Lema atashawishi watu kuvamia makazi
ya watu.
No comments:
Post a Comment