Hii ndio barabara ya rengue inayotokea mnara wa saa kuelekea TANESCO mpaka TRA ambapo utapeli huo hufanyika.
MOSHI Siku za hivi karibuni umeibuka utapeli wa kimazingira
ambapo umekuwa tishio sana kwa wakazi wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Kumekuwa na tabia za baadhi ya watu ambao
mpaka sasa majina yao hayajafahamika ila wamekuwa wakionekana sana maeneo ya barabara ya rengua mjini Moshi karibu na zilipo
ofisi za Tanzania Revenue Authority (TRA) mjini Moshi, National Microfinance Bank (NMB) na Ofisi kuu
za shirika la umeme Tanzania TANESCO.
Watu hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watano wanapotaka
kumtapeli mtu ni kwamba mmoja wao humsogelea mtu huyo wanayetaka kumtapeli na
kumsalimia na kujifanya yeye ni mgeni na anaulizia sehemu fulani baada ya
kuuliza sehemu hiyo wakati huo wale wenzake huwa maeneo ya karibu. Unapomaliza
kumuelekeza tapeli huyo sehemu aliyokuuliza anachokifanya ni kukushukuru kwa
kukushika mkono na wewe bila hiana unapompa mkono akikuachia kama ni mwanamke
utafungua pochi yako mwenyewe na kumtolea hela na kama ni mwanaume utaingiza
mkono mfukoni na kutoa pesa na kumkabidhi.
Baaada ya hapo matapeli wale hukodisha tax au pikipiki
maarufu kama bodaboda na kutokomea pasipojulikana na kumuacha aliyetapeliwa
akiwa kama vile amepigwa na butwaa na baada ya dakika chache akili za mtu
aliyetapeliwa hurudi sawa na kutambua kuwa ameshatapeliwa pesa zake. Baada
tukio hilo kufanyika kinachofuata ni mtu yule aliyetapeliwa kuanza kusikitika
au wengine hupiga mayowe ya kuhitaji msaada kutoka kwa wasamaria wema kitu ambacho
huwa ni kigumu sana kupata msaada maana matapeli wale wanakuwa wamesha tokomea
pasipo julikana.
Na siku za hivi karibuni mama mmoja alikumbwa na utapeli huo
ambapo yeye alitoka kuchukua kiasi cha shilingi milioni tatu pale National
Microfinance Bank (NMB), na anasema yeye
alikutwa na utapeli huo baada ya kufatwa na kijana/tapeli mmoja aliyejifanya
mgeni na kumuomba amuoneshe zilipo ofisi za mabasi ya Dar Express na mama
alimuelekeza kijana yule baada ya hapo yule kijana/tapeli alimshukuru yule mama
na kumpa mkono wa ahsante na hapo yule mama alifungua pochi na kutoa kiasi cha
shilingi milioni tatu na kumkabidhi kijana/tapeli yule. Baada ya hapo kijana yule aliita tax na
kutokomea pasipojulikana.
Kwa mujibu wa watu waliopo maeneo unapofanyikia utapeli huo wanasema matapeli hao huonekana sana tarehe za mwisho w
mwezi ambapo wanajua kuwa watu wengi huenda kuchukua pesa zao pale National
Microfinance Bank (NMB), na wengine huwa wanaenda kuchukua maelezo pale Tanzania
Revenue Authority (TRA) kwa ajili ya kwenda kulipa kodi mbalimbali za serikali.
No comments:
Post a Comment