Ni dhahiri kuwa muziki kwa Tanzania umekuwa ajira kwa vijana walio wengi sana pia umepunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa sana. Japo kila kazi inakuwa na changamoto zake ila leo tutaweza kufahamu mengi kuhusu changamoto wanazokutana nazo watayarishaji wa muziki hususani wa hapa Tanzania.
Jofa: Mambo vipi?
SAMTIMBER: Poa niaje mwana?
Jofa: Fresh sana.. Kuna baadhi ya watu hawakufahamu na
wangetamani kukufahamu, Je unaweza kujitambulisha wewe ni nani?
SAMTIMBER: Mimi ni mtanzania ambaye nimezaliwa jijini mwanza
almaarufu kama Rocky City mji wa mawe, pia ni mtayarishaji wa music (music
producer)na pia ni director ambaye nashoot music videos, documentary na projects
zote zinazohusu shooting, na kampuni yangu inaitwa SARTIMBER DIGITAL SOLUTIONS
ipo hapa hapa jijini Arusha.
Jofa: Hongera sana kaka.. Unaweza kukumbuka umeanza kazi za utayarishaji wa muziki lini?
SAMTIMBER: nimeanza mwaka 2004 nikiwa jijini Mwanza.
Jofa: Mpaka sasa unaweza kukumbuka umeshafanya nyimbo ngapi?
SAMTIMBER: Siwezi kukumbuka ni nyimbo ngapi, coz nimefanya kazi
mikoa mingi hapa Tanzania but ni songs nyingi sana.
Jofa: Unaweza kutaja baadhi ya nyimbo ulizofanya na zikaweza
kufanya vizuri?
SAMTIMBER: Neno ya Fid q na Lord Eyez, Nadhifa ya Sajna,
Nisikilize ya Dark Master ft. Chelea man, My city ya Geez mabov, Fido, JCB, Lavost
na Ibra da hasla.
Jofa: Unaweza kuuzungumziaje muziki wa Tanzania kwa ujumla?
SAMTIMBER: Yea music uko tyte sana sema wadau ambao ni
promoters na managers wameweka nguvu dar. but music wa Arusha uko real sana coz
ndo maisha wanayoishi.
Jofa: Nyimbo ya msanii inaposhindwa kufanya vizuri unadhani
nani anatakiwa kulaumiwa kati ya producer na msanii?
SAMTIMBER: Promoters ndo wanafanya music upande pia na media
ndo za kulaumiwa.
Jofa: Kwanini zilaumiwe media wakati au promotors wakati
producer ndio ameshirikiana na msanii wakatengeneza nyimbo mbaya?
SAMTIMBER: nyimbo mbaya ni asilimia10, but hata ikiwa mbaya
kwenye promo ndo kila kitu, bidhaa yoyote lazima ifanyiwe matangazo kwa mfano
bia, soda au mitandao ya simu ni vitu ambavyo kila mtu anavifahamu lakini kila
siku vinafanyiwa matangazo kwenye media.
Jofa: Unaushauri gani kwa wasanii wa Arusha na wengine walio
nje ya Arusha?
SAMTIMBER: Music ni kazi kama kazi zingine na biashara ingine,so yatupasa kubuni njia sahihi ya kutengezea pesa kwa kutumia music, but pia
wasanii wasitegemee music peke yake, wanaweza kuwekeza katika biashara zingine
huku wakiwa wanafanya music wakati huo huo.
Jofa: Ni changamoto gani ambazo unakutana nazo katika utayarishaji wa muziki?
SAMTIMBER:kwenye audio ukweli wasanii wengi hawana pesa ya kuweza kurecord,so usipomrecord hana pesa inakua beeef mtaani,then kwenyue video wasanii wengi hawawezi lipia gharama za kufanya video coz hawana ajira.
Jofa: Ni producer gani unamkubali sana?
SAMTIMBER: Mimi binafsi kibongo bongo namkubali sana Dunga wa
mandugu digital, coz ni producer ambaye anapiga kazi nzuri na pia hafeck life
kwa maana ya kwamba, hana majivuno si mbinafsi wa kutoa taaluma yake kwa mtu
yoyote halewi sifa kama star, anaweza kuchat na mtu yoyote haangalii rika,
ustar wala udini, kimbelembele namkubali sana Dr Dre hiphop is my life.
Jofa: Kwa wasanii walioko nje ya Arusha wanawezaje kukupata au kuwasiliana na wewe ili kufanya na wewe kazi?
SAMTIMBER: email yangu ni.jumpersamtimber@yahoo.com.simu ni .0716131666,0756825515 facebook account ni.samtimber jumper
Samtimber akiwa Fnouk Studio iliyopo jijini Arusha.
Mbele ni Spac Dawg, Samtimber na Riky wayne
Kumbukumbu nzuri kati ya Samtimber na Jofa.
No comments:
Post a Comment