Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, Bw. Leonidas Gama.
Mkoa wa Kilimanjaro unatarajia kujenga mji wa viwanda na biashara katika eneo la Lokolova ili kuchochea uongezaji thamani mazao na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nchi jirani.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, Bw. Leonidas Gama aliwaambia waandishi wa habari
hivi karibuni mjini Moshi kuwa eneo hilo ambalo tayari limebainishwa
litatoa fursa kubwa ya biashara.“Serikali
ya Mkoa kwa kushirikiana na sekta binafsi tumepanga mipango hii ili
kuboresha biashara,” alisema, na kuongeza kuwa eneo hilo litajengwa
viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.
Alisema
mji huo utakuwa nguzo kubwa kwa soko la kisasa la kimataifa
linalotarajiwa kujengwa katika eneo hilo la Lokolova kwa ajili ya masoko
ya ndani na nje ya nchi.“Mkoa
wetu huu upo mpakani na ni mashuhuri sana katika biashara lakini bado
tunauza mazao ambayo ni ghafi ambayo hayana tija kubwa ya kibiashara,”
alisema.
Alisema
kama ilivyo katika maeneo mbalimbali nchini, bado wananchi wa mkoa huo
wanauza mazao ghafi na kuwa ujio wa viwanda hivyo utasaidia kusindikwa
kwa mazao hayo na hivyo kuleta tija zaidi.Alibainisha
kwamba wakati wa kuuza mazao ghafi umepitwa na wakati, hivyo mipango
hiyo imekuja katika kipindi sahihi ambapo mazao yataongezwa thamani na
kupangwa katika madaraja ili kupata soko zaidi.
Mkoa huo ni maarufu kwa mazao mbalimbali kama nyanya, ndizi, maparachichi na mbogamboga.Akizungumzia
mradi mwingine alisema katika wilaya ya Siha wanatarajia kuanzisha
kituo kikubwa cha kisasa cha utalii ili kuongeza utalii katika mkoa wao.
“Kituo hiki kitajengwa
katika maeneo yaliyokuwa ya Serikali ambayo kwa sasa hayatumiki, na
kujengwa vivutio vizuri vya utalii mbalimbali,” alisema.Kwa
mujibu wa Bw. Gama, mpango huo ukikamilika utaongeza idadi ya watalii
na kusaidia kukuza mapato ya sekta binafsi na umma na kukuza uchumi wa
nchi.
Alifafanua
kuwa vivutio vitakavyojengwa ni pamoja na eneo la maonyesho, bustani
mbalimbali ikiwemo ya wanyama, maua, mahoteli ya kisasa na maeneo ya
michezo.Pia
utajegwa mfano wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya watalii ambao hawawezi
kwenda kuona na kuupanda mlima huo maarufu barani Afrika.
Alisema miradi yote hiyo itafanywa kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na biafsi kwa faida ya pande zote mbili.Alisistiza
kuwa mkoa wake na halmashauri zote zimebainisha maeneo ya biashara na
kuyatenga ambapo sekta binafsi itayatumia kufanya biashara bila vikwazo
vyovyote.
Chanzo: Michuzi blog
No comments:
Post a Comment