KILIMANJARO tume ya vyuo vikuu nchini, (TCU), imekipandisha hadhi chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara mkoani Kilimanjaro MUCCoBS kuwa chuo kikuu kamili kitakachojulikana kama chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU).
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha
Sokoine cha kilimo Philemon L. Luhanjo, wakati wa hafla ya kutangaza mabadiliko ya
chuo kikuu kishiriki cha ushrika Moshi, (MUCCoBS).
Aidha Luhanjo alitangaza mabadiliko makubwa katika chuo kikuu
hicho kipya kuanzia Julai 3, mwaka huu ambapo alisema ni pamoja na jina la chuo
hicho kuwa chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU).
Aidha alisema kuwa katika uteuzi huo Prof. Gerald Monele
ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la mpito la MoCU, ambapo Prof. Faustine
Bee, ameteuliwa kuwa kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu hicho kipya.
Akizungumza katika hafla hiyo, mwenyekiti wa baraza la mpito
la chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU), Prof. Gerald Monela, aliahidi
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukamilisha yale yaliyo ambayo serikali
inategemea yafanyike.
No comments:
Post a Comment