KILIMANJARO chama cha Akiba na Mikopo cha
wakulima wa mpunga (CHAMIWAMKA), cha eneo la Kaloleni, manispaa ya
Moshi, mkoani Kilimanjaro, kimeazimia kutafuta masoko ya nje ya mazao yao.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti
wa chama hicho Bw. Maulid Athuman, wakati wa semina ya mafunzo kwa wanachama wa
chama hicho pamoja wakulima wa mpunga ambao si wanachama wake, iliyofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, hivi karibuni.
“Ili kutimiza azma yetu,
uongozi wa chama chetu umeanza mikakati ya kuomba leseni kwa ajili kuuza nje ya nchi mpunga
tunaozalisha ili kukiongezea chama chetu na wanachama wetu mapato”,
alisema Bw. Maulid Athuman,.
Aidha Bw. Abdhalla alisema
chama hicho pia kimeanza mikakati ya kuanzisha miradi mingine ambayo itasaidia
kukiongezea chama hicho mapato pamoja na wakulima ambao ni wanachama wa chama hicho.
Akiongea katika semina hiyo,
mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Ahsanterabi Msigomba kutoka benki ya ushirika
mkoani Kilimanjaro, KCBL, alisema kuwa chama hicho tayari kinafanya kazi na
vyama vya ushirika 238, vikiwemo vile vya akiba na mikopo, (Saccos), vyama vya
kilimo na masoko, (Amcos), pamoja na vyama vikuu vya ushirika mkoani Kilimanjaro, vya
KNCU na Vuasu.
“Ushirikiano wetu wa
kibiashara na vyama hivi umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo nitoe rai
kwa wale wakulima ambao hawajajiunga na CHAMIWAMKA kufanya hivyo ili waweze
kufaidi ushirikiano huu”, alisema Bw. Msigomba.
Aidha alitoa rai kwa wakulima
na wafanyabiashara kuepuka dhana potofu kuwa mikopo huwa inafilisi ambapo
alisema mikopo huinua na kuboresha maisha ya wale wote wenye kuitumia kama
ilivyo kusudiwa.
No comments:
Post a Comment