KILIMANJARO zaidi ya vyama takribani 48 vya msingi vya wakulima wa zao la kahawa mkoani Kilimanjaro vimeshindwa kuingia katika
mfumo mpya wa uuzaji na ukusanyaji wa zao hilo ulioletwa na serikali kutokana sababu
mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mitaji.
Hayo yalibainishwa na Meneja Mkuu wa chama kikuu cha ushirika
cha wakulima wa zao hilo mkoani Kilimanjaro (KNCU) Onest Temba, wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini moshi mkoani hapa.
Temba alisema kati ya vyama vya msingi 64 vya wakulima wa
kahawa, vyama 9 ndivyo vilivyoweza
kuanza kutumia mfumo mpya huku vingene 48 vikishindwa kusimama vyenyewe
kutokana na ukosefu wa mitaji.
Aidha alisema ili kuvilinda vyama vilivyoshindwa visife na
viendelee kufanya kazi KNCU itaendelea kuwa na vyama hivyo mpaka pale vitakapo
kuwa na uwezo wa kusimama vyenyewe na
kujitegemea kufanya biashara hiyo kama
ilivyo kwa vyama vingine.
Alisema pamoja na vyama hivyo kuingia katika mfumo huo mpya
bado vitaendelea kuleta ushuru KNCU na kwamba mfumo huo hauzuii KNCU
kujikusanyia mapato yake kutoka katika vyama hivyo.
Kutokana na hali hiyo Meneja huyo aliwataka viongozi wa vyama
hivyo kuwa makini kutokana na kwamba pasipo kuwa na utendaji na usimamizi mzuri
kunauwezekanao mkubwa wa kuanguka kutokana na gharama za mikopo ya benki.
Alisema ni vema vya hivyo kuchukua mikopo kutoka benki
kwaajili ya kufanya biashara hiyo na kuleta faida na kwamba kuchukua fedha na
kuto timiza malengo waliyoyakusudia ni chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa vyama hivyo.
No comments:
Post a Comment