KILIMANJARO raia wa
nne kutoka nchini Ethiopia wanashikiliwa
na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa wakiwa wamejificha
vichakani.
Kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, amethibitisha kukamatwa kwa raia hao na
kwamba walikamatwa tarehe 19 Novemba mwaka 2014, majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha
Kileo wilayani mwanga.
Kamanda Kamwela
alisema raia hao walikamatwa wakiwa katika vichaka vya kijiji hicho
wakihangaika kutafuta njia ya kupita.
Kamwela alisema
katika upekuzi uliofanywa kwa raia hao hawakukutwa na chochote wala nyaraka za kusafiria walikuwa
hawana.
Alisema raia
hao wametokea nchini Kenya na kuingia nchini kwa kutumia njia za panya na
kwamba walikuwa wakipita kuelekea nchini
Afrika Kusini.
Kamanda aliwataja
wahamiaji hao kuwa ni Tamru Haile(20) Adinal Samwel (17) Tekele Gebure (17) na Solomon Adise (18) ambapo waliingia nchini
kinyume cha sheria.
Alisema kukamatwa
kwa raia hao kumetokana na wananchi waliowaona
na kuwatilia mashaka na kutoa taarifa kwa askari.
No comments:
Post a Comment