Mashindano  ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo  yanatarajiwa kutizamwa na watu wanaokadiriwa kufikia million 200  kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.
  Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo  yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani  City,  jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama  ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo  hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.
  Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto  wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za  ukanda wa afrika mashariki.
 Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania,  Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni  pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi,  pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na  Mauritius.
  Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na  kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa  Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu  wa Afrika
  Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza  wawakilishi wake ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan,  Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza  wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi  September.
  Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.




No comments:
Post a Comment