Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 27, 2014

Video mpya kutoka kwa YOUNG SUMA - "ME NI STAR" chini ya Mausay Records

ZAIDI YA MILIONI 120 ZINAHITAJIKA ILI KUFANIKISHA “Mount Kilimanjaro Festival”




KILIMANJARO zaidi ya Shilingi Milioni 120 zinahitajika ili kukamilisha Tamasha la Biashara, Utamaduni na Michezo (Mount Kilimanjaro Festival) linalotarajiwa kufanyika Desemba 17-23 mwaka huu mkoani Kilimanjaro.


Pia Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kusema katika ufunguzi wake mwaka huu watakuwa na msanii maarufu wa nyimbo ambaye hakutaka jina lake litajwe na timu ya daraja la kwanza au Ligi kuu itayoweza kutoa burudani kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandilizi ya Tamasha hilo  Patrick Boisafi alisema Desemba 17-23 ni kilele cha shughuli nzima itakayoanza kufanyika katika wilaya nane za mkoa wa Kilimanjaro ili kutafuta vikundi na timu mbalimbali.

“Kibiashara tamasha hili litasaidia kukuza uchumi, utamaduni na michezo, pia vitatoa hamasa kwa vijana chipukizi lakini litahusisha vikundi na timu za serikali za mitaa, ili kunogesha zaidi, hivyo maandalizi yanatakiwa kuanzia wilayani hadi siku ya kilele”.

Aidha alisema vikundi na timu hizo zinatakiwa kuandaliwa ipasavyo ikiwemo michezo ya bao, ngoma, kukimbia kwa magunia, kuvuta kamba, mpira wa pete, mpira wa miguu na mpira wa wavu.

Kauli mbiu ya Mt. Kilimanjaro Festival ni “ Biashara, Utamaduni na Michezo, kujenga uchumi wa Kilimanjaro”.
Na Jabir Johnson

Monday, August 25, 2014

Mkurugenzi mtendaji wa Panone "Patrick Ngiloi Ulomi" akiipokea timu ya Real Madrid


  Mkurugenzi mtendaji wa Panone Patrick Ngiloi Ulomi





   Mkurugenzi mtendaji wa Panone Patrick Ngiloi Ulomi akiongea na Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Fenella Mukangara







  Mkurugenzi mtendaji wa Panone Patrick Ngiloi Ulomi akimkabidhi zawadi Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Fenella Mukangara ili aweze kuikabidhi timu ya Real Madrid





   Mkurugenzi mtendaji wa Panone Patrick Ngiloi Ulomi wakiwa katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ( KINAPA)









 











Friday, August 22, 2014

ZIARA YA MAGWIJI WA MPIRA ULIMWENGUNI REAL MADRID MKOANI KILIMANJARO

d8f4b35c644f0423a21a23076ac82592
Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima enzi hizo wakicheza Real Madrid - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3927#sthash.mdYMdq4X.dpuf
Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima enzi hizo wakicheza Real Madrid - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3927#sthash.mdYMdq4X.dpuf
Kutoka kulia ni Ronaldo De Lima, Zinedine Zidane na Luis Figo, enzi wakichezea Real MAdrid
Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima enzi hizo wakicheza Real Madrid - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3927#sthash.mdYMdq4X.dpuf

Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima enzi hizo wakicheza Real Madrid - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3927#sthash.mdYMdq4X.dpuf
MOSHI timu ya Real Madrid ya nchini Hispania, inatarajia kuwasili mkoani Kilimanjaro, Agosti 24, mwaka 2014 lengo likiwa ni kutangaza fursa za utalii zilizopo mkoani Kilimanjaro hususani katika mlima Kilimanjaro. 

Akitoa taarifa kwa wanahabari mkoani Kilimanjaro, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema ziara ya wachezaji hao itatoa mwanya kwa wachezaji wengine kuja hapa nchini Tanzania na kuweza kuzitembelea hifadhi zilizopo hapa nchini.

Alisema uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamejiandaa vyema katika kuwapokea wachezaji hao, na kuongeza kuwa mkoa umejiandaa vyema katika kuwakarimu wachezaji hao wa Real Madrid.

Gama alisema kuwa licha ya wachezaji hao kuja na kutembelea hifadhi ya mlima Kilimanjaro pia itatoa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro, na kwamba mkoa umeandaa ratiba ambayo itawafikisha hadi kwenye mlima Kilimanjaro na kupata maelezo kuhusu mlima mrefu kuliko yote barani Afrika.

Pia mkuu wa mkoa alisema baada ya kufika eneo la mlima Kilimanjaro, watapata fursa ya kupanda kwa umbali kidogo ili kujionea mandhari ya mlima huo jinsi ulivyo kisha kupata maelezo ya jinsi safari ya kuanza kuupanda mlima huo inavyofanyika.

Aidha alifafanua kuwa uongozi wa mkoa umeuagiza uongozi wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), kuandaa maelezo yatakayowawezesha wachezaji hao kushawishika kurudi tena kama watalii. Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya wachezaji hao baada ya kupanda mlima Kilimanjaro, watapata chakula cha mchana kabla ya kurudi mjini Moshi ambapo wanatarajia kuwa wageni rasmi katika mechi ya kirafiki kati ya mabingwa wa mkoa wa Kilimanjaro Panone FC na timu ya soka ya Machava ya mjini Kilimanjaro.

DIWANI WA KATA YA MASAMA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI.

HAI baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro limemchagua Ally Mwanga ambae ni Diwani wa kata ya Masama Mashariki (CCM) kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuanzia Julai 2014 hadi June 2015. 
Mwanga alichaguliwa kwa kupigiwa kura za siri za ndio au hapana baada ya mgombea wa Chama cha Demokransia na Maendeleo (CHADEMA) kujitoa kutokana na maridhiano walikubaliana wajumbe wa baraza hilo linaloundwa na vyama viwili vya Siasa vya CCM na CHADEMA. Uchaguzi huo wa kumchagua makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ulifanyika katika ukumbi wa Halamashauri ambapo vyama hivyo viwili vilikubaliana nafasi ya makamu mwenyekiti iendelee kushikiliwa na diwani wa CCM kutokana na kuongozwa na Mwenyekiti anayetoka CHADEMA. Awali akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Melekzedeck Humbe alisema Mwanga alipata kura 18 kati ya 19 zilizopigwa huku moja ikiharibika. Baraza hilo la madiwani pia liliwachagua wajumbe na wenyeviti mbalimbali wa kamati watakao ongoza kwa pindi cha mwaka mmoja cha kuanzia Agosti 2014 hadi June 2015.

Thursday, August 21, 2014

Downloa na Kusikiliza Wimbo wa ODEO ft. RUFF G - Wanibembeleza, (NOIZ)


Muite ODEO, Msanii chipukizi katika Game la muziki anakuja na wimbo "WANIBEMBELEZA" akiwa na Ruff G toka Nyutro Fellaz kwenye Chorus, bofya HAPA kupata WIMBO na kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na ODEO kwa nambari +255 757 041 671.

WATANZANIA WASHAURIWA KUJIENDELEZA KIELIMU KWA KUPITIA VYUO VIKUU HURIA

Wananchi, watumishi wa umma na mashirika binafsi  hapa nchini Tanzania wameshauriwa kujiunga katika vyuo vikuu huria vilivyopo hapa nchini ili waweze kujiongezea elimu itakayo wawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi  sambamba na kumudu ushindani wa soko la ajira.

Rai hiyo imetolewa na rais wa wanafunzi wa chuo kikuu huria cha mjini Moshi Bw. Adinani Kingazi ,walipotembelewa chuoni hapo na makamu mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Tolly Mbwette, ambapo amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa ,kuna umuhimu wakujiendeleza kielimu.

Bw. Kingazi alisema njia pekee ambayo itakayoweza kumkomboa mtumishi wa umma ama sekta binafsi kukabiliana ipasavyo katika soko la ajira ni kusoma katika chuo kikuu huria, ambapo kinampa fursa ya kusoma bila kuathiri shughuli zake za kiutendaji.

 Makamu mkuu wa chuo kikuu huria nchini Bw. Tolly Mbwette alisema serikali imeanza kuboresha baadhi miundombinu ikiwemo majengo katika vyuo vikuu huria hapa nchini pia katika kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa ina mpango maalumu wa kuhakikisha  kuwa inajenga vyuo vikuu huria nchi nzima.

Tuesday, August 19, 2014

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA CHIDD BENZ ft. DIAMOND & AY - "MPAKA KUCHEE"




MAJAMBAZI WAMUUA MLINZI KIKATILI NA KUPORA MALI

MOSHI  watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamempiga mlinzi wa jengo la  Lyamuya Constraction, Musa Muhamed (52) mkazi wa Mabogini, na kitu kibutu kichwani na kusababishia kufariki dunia, pamoja na kuvunja maduka mawili yaliyopo katika jengo hilo la Lyamuya Constraction.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea usiku wa kuamkia agusti 18  mwaka 2014 , katika mtaa wa kaunda, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo watu hao waliingia katika jengo hilo na kumpiga mlizi huyo na kitu kizito kichwani.

Boaz alisema baada ya kumpiga mlizi huyo watu hao walim'buruta hadi sehemu ambapo magari ya jengo hilo huegeshwa na kuutelekeza mwili wa marehemu.

Alisema watu hao baada ya kufanya unyama huo walivunja maduka  mawili  ambapo waliiba tarakilishi “Computer” mbili na vitu mbalimbali ambavyo thamani yake hajaweza kufahamika kwa haraka.

Kamanda Boaz, alisema walivunja duka la mimea na mifugo na kuiba tarakilishi “Computer” na vitu vingine ambavyo havija tambuliwa na wahusika ambapo alisema pia walivunja duka la vifaa vya umeme ambapo pia waliiba tarakilishi “Computer” na vifaa mbalimbali vya umeme.

Boaz alisema hakuna anaeshikiliwa hadi sasa na kwamba uchunguzi unaendelea ili  kuweza kuwatia nguvuni waliofanya tukio hilo, na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi.

Friday, August 15, 2014

WAZAZI WATAKIWA KUWA WAZALENDO KATIKA KULIPA ADA KWA AJILI YA WATOTO WAO

HAI wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwa wazalendo wa katika kulipa ada ya shule kwa watoto wao ili kuwapa watoto fursa ya kupata elimu kama ilivyo kusudiwa.

Swala hilo muhimu liliongelewa na Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Hai, Bw. Julius Kakyama, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya kibaoni kwenye kikao kilicho fanyika hivi karibuni katika ofisi ya mtaa wa kibaoni kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi.

Kakyama alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiwapeleka watoto wao shuleni kwa lengo na kusoma lakini likija suala la kuchangia chakula mashuleni wamekuwa wakaidi sana, jambo hilo la kutokutaka kutoa michango ya shule linarudisha elimu nyuma, hivyo amewaomba wazazi wilayani humo kuchangia chakula  kwa wingi mashuleni ili wanafunzi waweze kufaulu, kwani wanafunzi kukosa chakula  kunawafanya kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Alisema kuwa anatambua mchango mkubwa toka serikalini wa ujenzi wa shule na mabweni kwa shule ya sekondari Hai Day unaoendelea kufanyika pamoja na juhudi za wananchi katika kutoa michango yao kufanikisha ujenzi huo.

Akizungumzia suala la maabara katika shule ya sekondari Boma alisema kuwa wametoa ushirikiano katika ujenzi kwa fedha za TASAF  mwaka 2007 na kukamilisha madarasa.

Ameongeza pia mwaka 2011 walitumia fedha zilizo tolewa na TASAF na kujenga vyoo vya shule ambapo pia vilikamilika na kusema kuwa katika suala la ujenzi wa  maabara kuna mpango unaoandaliwa na halmashauri ya kuandika barua kwa watendaji kata ili waweze kufanyia mchakato suala hilo la ujenzi wa maabara.

WANANCHI WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU ZA AFYA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA

HAI wananchi wa mtaa wa kibaoni, kata ya  Hai mjini, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamelalamikia utaratibu na huduma zinazotolewa na hosipitali ya wilaya ya Hai kuwa haziridhishi na wananchi hao kulalamikia kudorora kwa huduma muhimu kama ya afya.

Wananchi hao wametoa malalamiko hayo hivi karibuni wakati wa mkutano wa  hadhara uliofanyika katika ofisi ya Mtaa wa Kibaoni na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Hai  Novatus Makunga, pamoja na wakuu wa idara wa wilaya ya Hai,  katika kusikiliza  kero mbalimbali za wananchi.

Baadhi ya kero ambazo wananchi hao walizitoa mbele ya mkuu wa wilaya ni pamoja na lugha chafu kwa baadhi ya wauguzi, muda mrefu wa kusubiri huduma mapokezi pamoja na ukosefu wa dawa tatizo linalo leta kero kwa wagonjwa.

Awali akisoma risala kwa mkuu wa wilaya mwenyekiti wa mtaa wa kibaoni ambaye ni diwani wa viti maalumu Amina Swai,  alisema kuwa  wagonjwa wamekuwa wakikosa dawa hospitalini hapo na kuelekezwa  kununua dawa hizo katika maduka ya dawa yanayomilikiwa na watu binafsi.

Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Felista Ritte, alikiri kuwepo kwa kero hizo hospitalini hapo na kusema kuwa tayari kuna watu na kitengo maalumu cha kusikiliza kero na kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwachukulia sheria kali kwa wauguzi na madaktari watakao kiuka wajibu wao kwa wagonjwa.

Ameongeza kwa kuwataka  wananchi hao kuwa wazalendo wa kuepuka gharama kubwa za kulipia matibabu kwa kuwataka kukata bima ya afya ili kuwarahisishia kupata matibabu.

Friday, August 8, 2014

KESI YA MAREHEMU MTOTO "NASRA RASHID MVUNGI" YAPIGWA TENA TAREHE

Kutoka kushoto ni aliyekuwa mlezi wa marehemu mtoto Nasra Rashid, Bi. Mariam Said  baba yake na Nasra, Bw. Rashid Mvungi na mume wa Bi. Mariam Said, Bwana Mtonga Omary.

Watuhumiwa Bw. Rashid Mvungi pamoja na waliokuwa walezi wake, Bi. Mariam Said na mumewe Mtonga Omary, wakiwa mahakamani.


Umati wa watu waliokuja kusikiliza kesi ya marehemu mtoto Nasra, wakiwa nje ya mahakama.

MOROGORO washtakiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji dhidi ya mtoto Nasra Rashid Mvungi, wamelazimika kubadilishiwa hakimu baada ya hakimu ambaye kesi yao imekuwa ikifikishwa mbele yake kwaajili ya kutajwa, kupata dharura na kutokuwepo mahakamani hapo.

Washtakiwa hao ambao kesi yao imekuwa ikifikishwa na kutajwa, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, Mary Moyo,  wamelazimika kupandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Agripina Kimanze na kusomewa mashtaka yao, baada ya hakimu Moyo kutokuwepo mahakamani hapo.

Kufuatia hali hiyo, washtakiwa hao walichelewa kupanda kizimbani tofauti na nyakati nyingine, hali iliyoonekana huenda ilisababishwa na mabadiliko hayo ya kukosekana kwa hakimu husika.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Aminatha Mazengo, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba jalada bado lipo kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali, hivyo kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Mahakama imeridhia ombi hilo, na kupanga Agosti 20 mwaka 2014, kufikishwa tena kwa kesi hiyo kwaajili ya kutajwa, kutokana na mahakama hiyo kukosa uwezo kisheria kusikiliza shtaka la mauaji  huku washtakiwa wakirudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo ya mauaji inawakabili washtakiwa watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto Nasra, Bw. Rashid Mvungi pamoja na waliokuwa walezi wake, Bi. Mariam Said Na mumewe Mtonga Omary, ambao awali walikuwa wakikabiliwa na shtaka la kula njama na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya Mtoto Nasra Mvungi kabla ya baadaye mashtaka yao kubadilishwa na kuwa ya mauaji baada ya mtoto huyo kufariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UKATILI KWA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI

KILIMANJARO mkazi mmoja wa Singida mjini aliyefahamika kwa jina la Jackline Kweka (30) jana alipandishwa Mahakama ya wilaya ya Hai akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani mwenye umri wa miaka 15.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akimpiga mfanyakazi wake huyo sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo kumvuta nyama za siri kwa kutumia plaizi.

Baada ya tuhuma hizo kuibuliwa na raia wema mtuhumiwa huyo alitoroka kutoka mkoani Singida na kukimbilia katika kijiji cha Narumu wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro alikokamatiwa baada ya taarifa kuvuja.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani mbele ya hakimu mkazi, mfawidhi wa wilaya, Denis Mpelembwa na kukanusha mashitaka dhidi yake. Hati ya mashitaka hayo ni ya awali ili kuruhusu polisi kutoka Singida kwenda kumchukua mtuhumiwa huyo.

Akisoma mashitaka Mwendesha Mashitaka wa polisi, inspekta Marwa Mwita alidai mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo Julai mwaka 2014, kwa siku tofauti tofauti.

Mtuhumiwa huyo alikanusha mashitaka hayo na amerudishwa rumande hadi Agosti 21 mwaka 2014, wakati ukisubiriwa utaratibu wa kumsafirisha kwenda mkoani Singida.

Msichana anayedaiwa kufanyiwa ukatili huo alilazwa katika hospitali ya wilaya ya Hai kwa Matibabu na taarifa zinadai amepoteza uwezo wa kusikia na hapati tene siku zake za hedhi.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AWASHAURI WANANCHI KUJIWEKEA AKIBA YA CHAKULA

KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imewataka wananchi kujiwekea akiba ya chakula katika kipindi hichi cha mavuno na kuacha kutumia nafaka kwa kutengenezea pombe za kienyeji, lengo likiwa ni kukabiliana na kipindi cha njaa.

Mkuu wa mkoa wa kilimnjaro Leonidas Gama, aliyasema hayo wakati akizungumza na mmoja muandishi wa mtandao huu jana Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo alisema hali ya kilimo na upatikanaji wa chakula ni ya kuridhasha.

Alisema mkoa wa Kilimanjaro  baadhi ya wilaya zake zimekuwa zikikabiliwa na njaa kutokana  na wananchi kutokuwa na desturi ya kujiwekea akiba ya chakula katika kipindi cha mavuno na kutumia nafaka katika utengenzaji wa pombe za kienyeji.

Alisema  mkoa ulijiwekea malengo ya kuvuna na kukusanya zaidi ya tani Milioni 1.9 katika kipindi cha   mwaka 2013/2014 na kwamba hali ya upatikaji   wa chakula ni ya kuridhisha ambapo katika kipindi cha mwaka 2014 wanatarajia kuvuna kuvuka lengo hilo.
 
Aidha aliziagiza halmashauri za wilaya  kupitia wataalamu wa kilimo mkoani Kilimanjaro kuwaelimisha wananchi juu ya njia bora za kuhifadhi  mazao ili kusaidia vyakula hivyo kuto haribika kwa haraka.

Thursday, August 7, 2014

MKOA WA KILIMANJARO UMEFANIKIWA KUJENGA MAABARA ZAIDI YA 130

KILIMANJARO maabara zaidi ya 130 zimejengwa katika mkoa wa Kilimanjaro kwenye shule mbalimbali za sekondari, kwa lengo la kuboresha masomo ya sayansi katika shule hizo na mkoa huo kwa ujumla.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na agizo la Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, lililowataka viongozi wa mikoa yote Tanzania kuhakikisha kila shule ya sekondari inakuwa na maabara.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro alisema katika kutekeleza mpango huo kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya wananchi kuwa na ugumu wa kutokuwa na ushirikiano katika ujenzi wa maabara hizo ili kufanikisha zoezi hilo.

Aidha Gama aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikiwemo sekta ya elimu na kwamba mbali na juhudi za serikali michango inayotolewa na wananchi ni muhimu kwa ajili ya maendeleo.

Alisisitiza na kutoa wito kwa wanafunzi kuhakikisha wanajituma katika elimu ili kuenzi juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na wananchi katika kuchangia miradi ya elimu.

WANAKIJIJI WAMLALAMIKIA MUWEKEZAJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YA MKATABA KWA MIAKA 20



MOSHI wakazi wa kijiji cha Kitandu kata ya Uru kusini wilayani ya Moshi mkoani kilimanjaro wamemtaka mwekezaji wa shamba kubwa la kahawa lenye hekari 555 la kifumbu/kate kutekeleza makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa uwekezaji.

Wananchi hao walitoa agizo hilo katika mkutano  mkuu wa serikali ya kijiji uliofanyika tarehe 5 Augasti 2014 na kuudhuriwa na  wawakilishi wa mwekezaji wa kampuni ya Kilimanjaro  Plantation LTD. (KPL).

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Mwenyekiti wa Kijiji hicho Dominick Mushi, alisema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza mkabata huo kwa kushindwa kuwapatia huduma za kijamii wananchi kwa miaka 20.

Mushi alisema baadhi ya huduma hizo ni pamoja na maji, elimu, afya, barabara, ajira kwa wananchi na kudorora kwa ushirikiano kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wananchi wa kijiji hicho.

Aidha alisema, kwa muda mrefu serikali ya kijiji ilikuwa inauomba uongozi wa kampuni hiyo kukutana na wananchi kujadili mustakabali wa mkataba huo lakini viongozi wa kampuni wamekuwa hawatoi ushirikiano.

Alisema kwa zaidi ya miaka 20 ni mara ya kwanza kwa viongozi wa kamapuni hiyo kukaa na wananchi na kusikiliza kero zao zinazo wakabili likiwemo suala zima la maendeleo.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo Jacob De Haan aliahidi  kuwasilisha hoja za wananchi hao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Volker Schuckert ambaye kwa sasa yuko nchini Ujerumani kwa mapumziko na kwamba  matumaini yake kuwa zitafanyiwa kazi kwa mujibu wa mkataba.

Mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa kampuni hiyo Shaaban Deogratius alikiri uhusiano mbaya uliopo kati ya pande hizo na kuaahidi kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na kuondoa tofauti zilizojitokeza.

Shaaban alisema, katika hatua za awali aliahidi ajira 25 za ulinzi kwa vijana watakaomaliza mafunzo ya mgambo katika kijiji hicho ili kuziba pengo la walinzi waliopo ambao baadhi yao ni wazee na wengine hawana sifa.

Nao baadhi ya wananchi hao walikiomba chama cha msingi cha ushirika mkoani  Kilimanjaro kurejea katika mkataba huo upya kutokana na kwamba awali walitiliana saini na kampuni ijulikanayo kwa jina la T-CHIBO, lakini sasa kampuni iliyopo ni kilimanjaro Planters ltd.

“KIRUA VUNJO NORTH AMCOS” Yatarajia Kukusanya Shilingi Milioni 4.8 Kwa Mwaka 2014/2015

MOSHI chama cha ushirika wa masoko na mazao ya kilimo cha Kirua Vunjo Kaskazini, (Kirua Vunjo North Amcos) cha Moshi Vjijini, mkoani Kilimanjaro, kinatarajia kupata mapato ya ziada ya shilingi milioni 4.8 katika msimu wa 2014/2015.
 
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama hicho Bw. John Chaki, wakati akizungumza na wanahabari mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, hivi karibuni.
 
Ziada hii itatokana na mapato ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 15 tunayotarajia kuyapata katika kipindi hiki”, alisema na kuongeza kuwa wanachama wa chama hicho tayari wameridhia kujiunga na mfumo mpya wa kukusanya kahawa kwa kujitegemea.
 
Aliongeza, “Ili kufanikisha zoezi la kujitegemea katika mfumo huu mpya, wanachama wamepitisha ukomo wa madeni wa shilingi milioni 120 kutoka benki ya ushirika mkoani Kilimanjaro, (KCBL) kwa ajili ya kukusanyia kahawa katika msimu huu mpya”.
 
Awali meneja masoko wa KCBL Bw. Asanterabi Msigomba, alisema benki hiyo tayari imeshaandaa mikakati inayolenga kuviwezesha vyama vya ushirika wa masoko na mazao ya kilimo vilivyojiunga na mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani.

Aidha alitoa wito kwa vyama vya ushirika masoko na mazao ya kilimo kujenga tabia ya kuwalipa wakulima fedha zao punde wanapowasilisha mazao yao ili waweze kujiendeleza ikiwamo kulipa fedha walizokopa kwa ajili ya kuimarisha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao.
 
Kosa kubwa ambalo linaweza kudhoofisha juhudi za kilimo ni kutokumlipa mkulima kwa wakati na wakulima kuuza mazao nje ya mfumo wa chama, mambo haya hudhoofisha mfumo mzima unaolenga kuongeza tija katika kilimo”, alionya.
 
Bw. Msigomba pia alielezea umuhimu wa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani ulioasisiwa na benki hiyo ya kwanza ya ushirika hapa nchini ambapo alisema tayari taasisi hiyo ishatoa mafunzo kwa vyama vya ushirika wa masoko na mazao ya kilimo, (Amcos), kuhusu mfumo huo.